User Rating: 0 / 5

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 

Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF umeingia makubaliano na Ofisi ya waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) ya kutumia miundombinu ya Teknolojia ya habari na mawasiliano inayounganisha Halmashauri na Mikoa yote nchini.

Akizungumzia ushirikiano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga alisema kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa vile utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unatumia mifumo ya TEHAMA ambapo taarifa za walengwa huwekwa na kuchakatwa katika mfumo wa MIS kuwezesha kutambua, kutenganisha, kulipa ruzuku stahiki na kutunza kumbukumbu za walengwa.

"Kutokana na umuhimu huo, tulilazimika kufikiria namna ya kufanikisha hayo yote kwa kuangalia kwanza juhudi zilizopo za serikali katika matumizi ya mifumo ili kupunguza gharama na kutoanzisha mifumo" alisema Mwamanga.

Akianisha mafanikio yanayotarajiwa kutokana na matumizi ya miundombinu hiyo, Bw. Mwamanga alifafanua kuwa TASAF itafaidika kwa kupunguza gharama za uwekezaji katika kuweka mfumo, kupunguza gharama za uendeshaji kama vile ya malipo, kutumia muda mfupi wa utekelezaji wa zoezi la kuunganisha halmashauri na TASAF Makao makuu pamoja na kutumia wataalamu wa mifumo ya TEHAMA wa Halmashauri kutoa msaada wa kitaalamu kwa ofisi za TASAF zilizoko huko.

Kwa upande wake Katibu Mkuu OWM-TAMISEMI Bw. Jumanne Abdallah Sagini ameelza kuwa hadi sasa, Kituo kikuu cha kompyuta kilichopo Dodoma OWM-TAMISEMI kimefanikiwa kuunganisha halmashauri 133 na Mikoa 25 kwa miundombinu ya TEHAMA ambayo imekuwa kiungo kikuu cha mawasiliano kati ya ofisi hiyo na Mikoa, halmashauri, Wizarataasisi zingine mbalimbali.

"OWM-TAMISEMI ilizingatia vigezo na viwango vya kitaalamu kwakuwa utanuzi wake ni rahisi, imara na salama kwa matumizi na hivyo akazishauri taasisi zingine za serikali kutumia miundombinu ya mawasiliano ya TAMISEMI" alisema Sagini.

Tayari mfumo wa TASAF umezifikia hamashauri sitini zilizounganishwa katika miundombinu hiyo ambapo utaratibu wa matumizi yake umesaidia kuongeza ufanisi wa matumizi ya mfumo wa TASAF kwa kuweka taarifa za Halmashauri husika na kupatikana kwa taarifa, kupokea maelekezo na miongozo kutoka makao makuu kwa wakati.

pic1

Katibu Mkuu OWM-TAMISEMI Bw. Jumanne Abdallah Sagini (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga wakitia saini hati ya makubaliano (MoU) juu ya Matumizi ya miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inayounganisha Halmashauri na Mikoa yote nchini

pic2

Katibu Mkuu OWM-TAMISEMI Bw. Jumanne Abdallah Sagini (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano (MoU) na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga juu ya Matumizi ya miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inayounganisha Halmashauri na Mikoa yote nchini.

pic3

Baadhi ya watendaji wa TASAF wakishuhudia utiaji saini hati ya makubaliano (MoU) baina ya TASAF na OWM-TAMISEMI juu ya Matumizi ya miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inayounganisha Halmashauri na Mikoa yote nchini.

pic4

Baadhi ya watendaji wa OWM-TAMISEMI na EGA wakishuhudia utiaji saini hati ya makubaliano (MoU) baina ya TASAF na OWM-TAMISEMI juu ya Matumizi ya miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inayounganisha Halmashauri na Mikoa yote nchini.

pic5

Katibu Mkuu OWM-TAMISEMI Bw. Jumanne Abdallah Sagini (kushoto walioketi) na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (kulia walioketi wakiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji wa OWM-TAMISEMI,TASAF wa eGA baada ya kusaini hati ya makubaliano (MoU) juu ya Matumizi ya miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inayounganisha Halmashauri na Mikoa yote nchini

Add comment


Security code
Refresh