User Rating: 0 / 5

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 

Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini umeuvutia ujumbe kutoka Serikali ya Nigeria kutokana na mafanikio makubwa kwa walengwa yaliyopatikana katika kipindi kifupi cha utekelezaji.

Ujumbe huo uliokuwa nchini kwa wiki moja kubadilishana uzoefu na kujifunza namna ambavyo Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF unavyotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, ulipata furs ya kutembelea Walengwa katika Vijiji vya Wiliko na Izava wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Ukiwa katika kijiji cha Wiliko, ujumbe huo ulishuhudia taratibu za malipo ya ruzuku ya fedha kwa walengwa na kujionea bwawa lililojengwa kwa nguvu za walengwa kupitia miradi ya ajira za muda zenye lengo la kuwaongezea kipato katika kipindi kigumu.

Ugeni huo pia ulifitembelea kijiji cha Izava na kufanya mazungumzo na walengwa ambao walitoa shuhuda zao jinsi ambavyo wamenufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na wakaeleza kuwa kwa sasa maisha yao yamekuwa bora kulinganisha na kipindi cha kabla ya kuingia katika mpango.

Katika mazungumzo hayo, kiongozi wa ujumbe huo Bw. Peter Pafka alisema kuwa ziara yao imekuwa ya mafanikio kwa kuwa wamejionea kwa macho namna ambavyo mpango wa Kunusuru Kaya Maskini umefanya kazi kubwa ya kuinua hali ya maisha ya kaya duni na kuzijengea uwezo.

Zifuatazo ni picha za baadhi ya matukio katika ziara hiyo.

pic2

Sehemu ya wageni toka Nigeria wakifuatilia kwa Makini mawasilisho juu ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kutoka kwa Mkurugrnzi wa Programu za Jamii Bw. Amadeus Kamagenge na watendaji wengine wa TASAF (hawapo pichani)

pic4

Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Erick Kitali (aliyesimama) akiwasilisha namna ambavyo idara ya TEHAMA inavyofanya kazi katika kuhamisha fedha kwenda katika maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PAAs).

pic6

Walengwa katika Kijiji cha Wiliko wakicheza Ngoma wakati wa mapokezi ya ugeni kutoka Nigeria

pic7

Mkurugenzi wa Uratibu wa TASAF Bw. Alphonce Kyariga akitoa maneno ya utangulizi yahusuyo ziara ya ugeni toka Nigeria katika Kijiji cha Wiliko

pic9

Kiongozi wa msafara kutoka Nigeria Bw. Peter Papka akielezea lengo la ziara yao hapa nchini

pic11

Mlengwa katika kijiji cha Wiliko Wilaya ya Chamwino akitoa shukrani kwa TASAF kwa usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao umewajengea uwezo wa kumudu kupata mahitaji yao muhimu.

 pic13

Sehemu ya umati wa walengwa katika kijiji cha Wiliko wakifuatilia maelezo ya wageni kutoka Nigeria waliofika kijijini hapo kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu juu ya utekelezaji wa Kunusuru Kaya Maskini.

pic15

Kiongozi wa msafara wa ugeni kutoka Nigeria Bw. Peter Papka akizungumza na wakazi wa kijiji cha Izava huku Afisa toka TASAF Bw. Mohamed Msala akitafsiri lugha kwa pande zote.

pic16

Mlengwa katika kijiji cha Izava Wilaya ya Chamwino akitoa shukrani kwa TASAF kwa usimamizi mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao umewajengea uwezo wa kumudu kupata mahitaji yao muhimu.

Add comment


Security code
Refresh