User Rating: 0 / 5

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 

Uongozi wa Vyama vya Waandishi wa habari vya Mikoa umevutiwa na utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini baada ya kushuhudia maendeleo ya Walengwa katika vijiji vya Diozile na Tukamisasa kata ya Msoga Wilayani Bagamoyo.

Wakiwa katika ziara ya kutembelea na kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na TASAF chini ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, viongozi hao na waandishi wa habari waandamizi kutoka vilabu vya mikoa yote ya Tanzania bara pamoja na Unguja na Pemba walivutiwa na hali ya mabadiliko ya maisha ya walengwa kutoka katika uduni wa maisha na kufanikiwa kuwa na maisha bora yanayowawezesha kumudu mahitaji yao ya msingi.

Katika ziara hiyo, wanahabari hao waliweza kushuhudia Walengwa wa Mpango wakiwa wameanzisha na kuendeleza miradi midogo midogo ya ufugaji wa kuku, mbuzi na nguruwe pamoja na kilimo cha mazao ya chakula na biashara.

Wanahabari hao pia walitembelea bwawa la maji katika kijiji cha Diozile lililojengwa kwa utaratibu wa Miradi ya ajira za muda zinazowaongezea Walengwa kipato na kuwaondolea adha ya ukosefu wa maji kwa kuwapatia uhakika wa upatikanaji wa maji kwa mwaka mzima.

Zifuatazao ni baadhi ya picha za matukio mbalimbali wakati wa ziara hiyo ya wanahabari.

pic1

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga akizungumza na viongozi wa vilabu vya waandishi wa habari na waandishi waandamizi (hawapo pichani) waliotembelea TASAF kujionea shughuli mbalimbali za utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. Wengine (walioketi) ni Mkurugenzi wa Programu za Jamii wa TASAF Bw. Amadeus Kamagenge (kushoto) na Mkurugenzi wa kujenga Uwezo wa TASAF Bw. Fariji Mishael

pic2

Baadhi ya Viongozi wa vilabu vya waandishi wa habari wakifuatilia maelezo ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini toka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani) katika Ukumbi wa CEEMI jijini Dar es Salaam

pic3

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa vilabu vya waandishi wa habari na waandishi waandamizi waliotembelea TASAF. Wakurugenzi wengine waliopo kwenye picha hii ni ni Mkurugenzi wa Programu za Jamii wa TASAF Bw. Amadeus Kamagenge ( wa pili toka kushoto walioketi) na Mkurugenzi wa kujenga Uwezo wa TASAF Bw. Fariji Mishael (wapili toka kulia walioketi)

pic4

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Bi. Erika Yegella (wa nne kushoto waliosimama mbele) na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bi. Elizabeth Ngonyani  (wa tatu kushoto waliosimama mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa vilabu vya waandishi wa habari na waandishi waandamizi na watendaji wa TASAF walipofika katika ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo

   pic5

Baadhi ya viongozi wa vilabu vya waandishi wa habari wakipata taarifa za utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ulivyowezesha kufanikisha ujenzi wa bwawa la maji katika kijiji cha Diozile chini ya Miradi ya ajira za muda

pic6

Wakazi wa kijiji cha Diozile wakichota maji toka katika bwawa lililoendelezwa kwa njia ya  Miradi ya ajira za muda

 

 

Add comment


Security code
Refresh