User Rating: 5 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Active
 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umeshiriki katika maonyesho ya NANE NANE mkoani Dodoma ambako Mfuko huo ulitumia fursa hiyo kuelezea masuala mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli zake hususani Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini –PSSN.

Miongoni mwa masuala yaliyojitokeza na kuulizwa na wananchi waliopata fursa ya kutembelea banda la TASAF lililoko katika jengo la Ofisi ya Rais kwenye viwanja vya Nane Nane nje kidogo ya mji wa Dodoma ni pamoja na namna walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya Masikini wanavyopatikana huku pia wengine wakihoji kuwa baadhi yao wameachwa kuingizwa kwenye Mpango licha ya kuwa hali zao ni mbaya kiuchumi. Baadhi ya Walengwa waliomba suala la elimu ya namna ya kutumia fedha za ruzuku kwa ajili ya kukuza shughuli zao za kiuchumi lipewe kipaumbele.

Aidha walengwa wengine waliotembelea banda la TASAF waliomba ruzuku inayotolewa iongezwe ili waweze kukidhi mahitaji yao na kukuza shughuli za kiuchumi.

Dukuduku na tashwishwi za wananchi waliotembelea banda la TASAF zilijibiwa na Maafisa waliokuwapo kwenye maonyesho hayo na hivyo kuweka sawa mizania ya uelewa kwao .

Zifuatazo ni baadhi ya picha za wananchi waliotembelea banda la TASAF kwenye maonyesho hayo ya Nane Nane mjini Dodoma

 

pic1

 

pic2

 

pic3

 

pic4

Add comment


Security code
Refresh