User Rating: 1 / 5

Star ActiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 

Halmashauri 13 za Mikoa ya Njombe na Arusha zinaanza kunufaika na miradi ya kupunguza Umaskini ya OPEC Awamu ya tatu kwa Watu takribani Milioni 3.1 itakayotekelezwa kwa Miaka Mitatu kati ya January 2015 na Desemba 2017.

Hayo yameelezwa mapema leo hii na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, IKULU bwana Peter Ilomo wakati akizindua kikao kazi cha kwanza kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa Njombe juu ya utekelezaji wa miradi hiyo ya kupunguza umaskini kwa ufadhili wa OPEC awamu ya tatu.

Bw. Ilomo amesema kuwa Lengo la utekelzaji wa miradi hiyo ni Kuboresha upatikanaji wa huduma za kiuchumi na Kijamii kwa Kaya Maskini zilizotambuliwa na kuandikishwa katika Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri huzo.

Aidha Bwana Ilomo amesema kuwa katika mradi huo jamii zitatekeleza miradi ya elimu, afya na maji pale patakapoonekana pana upungufu wa huduma hizo .

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF amezitaja Halmashauri zitakazohusika kwa katika Mikoa hiyo kuwa ni Ludewa, Makete, Njombe, Wanging'ombe na Halmahshauri za Mji Makambako na Njombe ambazo zote ni za Mkoa wa Njombe na akazitaja za Mkoa wa Arusha kuwa ni Longido, Monduli, Ngorongoro, Arusha, Meru, Karatu na Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Pamoja na miradi ya kupunguza umaskini ya OPEC, TASAF pia inatekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika halmashauri zote nchini ikiwa ni pamoja na Unguja na Pemba na tayari.

Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali katika kikao hicho.

pic1

Mkurugenzi mtendaji wa TASAF akitoa maelezo ya utangulizi juu ya miradi ya kupunguza umasikini ya OPEC awamu ya tatu.

pic2

Katibu mkuu ofisi ya Rais Ikulu Peter Ilomo akizindua mkutano wa kazi juu ya utekelezaji wa miradi ya kupunguza umasikini ya OPEC awamu ya tatu Mjini Njombe leo

pic3

Kaimu mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba akielezea hali halisi ya utekelezaji wa  shughuli za TASAF katika mkoa wa Njombe

pic4

Meneja wa miundombinu mhandisi Elisifa kinasha akielezea madhumuni ya mkutano wa TASAF awamu ya tatu

pic5

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kazi wakisikiliza na kunukuu hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo toka kwa katibu mkuu ofisi ya Rais Ikulu bw.Peter Ilomo (Hayupo pichani)

pic6

Meneja wa fedha Bw.Godwin Mkisi akitoa mada juu ya uratibu wa kutuma fedha

pic7

Afisa wa uratibu toka TASAF bw.Quintus Kassese  akiwasilisha mada juu ya mpango wa kunusuru kaya masikini

pic8

Baadhi ya Watendaji wa TASAF  wakiandaa mahitaji katika mkutano huo

pic9

Katibu mkuu ofisi ya Rais Ikulu Peter Ilomo (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa kazi kutoka Halmashauri za mkoa wa Njombe

pic10

Katibu mkuu ofisi ya Rais Ikulu Peter Ilomo (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji toka TASAF.

Add comment


Security code
Refresh