User Rating: 4 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Inactive
 

Walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wameanza utekelezaji wa miradi ya ajira za muda na kisha kulipwa ujira katika miradi wanayoibua kwenye maeneo yao .

Walengwa wa vijiji kadhaa vilivyoko kwenye Mpango huo kikiwemo kile cha Mzuri na Kijini vilivyoko katika eneo la Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja wameanza kutengeneza barabara yenye urefu wa zaidi ya kilometa moja na vitalu vya miche ya miti ya asili na matunda katika eneo lao na kisha kulipwa fedha chini ya utaratibu ulioandaliwa na TASAF ambao ni moja ya mkakati  wa kuwaongezea kipato walengwa na kupambana na umaskini.

Akizungumza na timu ya waandishi wa habari waliotembelea eneo hilo Sheha wa eneo hilo Bwana Mwita Masemo Makungu amebainisha kuwa mpango huo umeitikiwa vizuri na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika eneo hilo na kuwa jitihada hizo za TASAF zimeamsha ari ya wananchi kujiletea maendeleo kwenye maeneo yao na kupunguza kero ya barabara iliyokuwa inawakabili.

Hata hivyo Bwana Makungu amesema pamoja na ushiriki wa wananchi kwenye kazi hiyo kupitia mpango wa ajira za muda bado wananchi hao wanakabiliwa na tatizo la vifaa na utaalamu hususani katika ujenzi wa barabara ambao unahitaji vifaa vizito ambavyo havipo kwenye maeneo yao na hivyo kuomba serikali kuona namna ya kukamilisha kazi hiyo.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za walengwa wa PSSN katika wilaya ya Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja wakishiriki katika kazi kupitia ajira za muda PWP

ajira-znz-pic1

Kazi ya ujenzi wa barabara katika kijiji cha Kijini -Makunduchi mkoa wa kusini Unguja ambayo ni moja
ya mkakati wa TASAF wa kuwaongezea kipato walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini kupitia
ajira ya muda PWP.

 

ajira-znz-pic2

Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na TASAF katika kijiji cha
Kijini Makunduchi mkoa wa kusini Unguja wakishiriki katika kazi zaujenzi wa barabara kupitia mpango
wa ajira za muda PWP

 

 

Add comment


Security code
Refresh