User Rating: 3 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar InactiveStar Inactive
 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF na wadau wa Maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi wameanza Mkutano wa kupitia mafanikio na changamoto za utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini,PSSN unaoratibiwa na Mfuko huo nchini.

Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango huo unaowahusisha wataalamu mbalimbali kutoka Taasisi za Fedha na mashirika ya misaada ya kimataifa utawawezesha pia wataalamu hao kutembelea maeneo kadhaa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini katika mikoa ya Dodoma, Lindi na Zanzibar.

Akitoa tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema tayari kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 13 kimetumika katika kutoka ruzuku kwa walengwa wa Mpango huo na kuwa katika maeneo ambako ruzuku hiyo imetolewa kumekuwa na mafanikio makubwa ya uboreshaji wa maisha ya kwalengwa wa mpango huo.

Kwa Upande wao wadau wa Maendeleo kutoka BENKI YA DUNIA , UNICEF,ILO, UNPF,na DFID,,wameonyesha kuridhishwa kwao na namna TASAF inavyotekeleza Mpango wa kunusuru kaya maskini na kuonyesha kuwa kazi hiyo itakamilimka kwa mafanikio makubwa .


Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali ya mkutano kati ya watendaji wa TASAF na wadau wa maendeleo.

11000067

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana Ladislaus Mwamanga akiongoza Mkutano wa wadau wa maendeleo na maafisa wa TASAF juu ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru Kaya maskini nchini ,PSSN ulioanza leo Jijini DSM,

035

Baadhi ya wadau wa Maendeleo wakiwa katika mkutano wa kutathmini utekelezaji wa shughuli za Mpango wa kunusuru Kaya Maskini, unaoratibiwa na TASAF.

11000025

Baadhi ya wadau wa maendeleo na watendaji wa TASAF wakiwa katika mkutano wa kutathimini utekelezaji wa mpango wa Kunusuru kaya maskini PSSN.

11000074

Baadhi ya wadau wa maendeleo wakiongozwa na mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, aliyevaa tai walipotembelea chumba cha kurekodi takwimu za walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini ambacho kimefungwa zaidi ya kompyuta 100.

 

Add comment


Security code
Refresh